It was less than a year after September 11, and I was at the Chicago Tribune writing about shootings and murders, and it was leaving me feeling pretty dark and depressed. I had done some activism in college, so I decided to help a local group hang door knockers against animal testing. I thought it would be a safe way to do something positive, but of course I have the absolute worst luck ever, and we were all arrested. Police took this blurry photo of me holding leaflets as evidence.
Ilikuwa ni chini ya mwaka mmoja baada ya Septemba 11, Na nilikuwa katika ofisi ya gazeti la Chicago Tribune Nikiandika kuhusu mauaji, ilinisababisha nijihisi Katika hali ya giza na kuelemewa Nilikuwa mwanaharakati nilipokuwa chuoni, Nikaamua kulisaidia kundi la maeneo ya kwetu Kuweka mabango kinyume na kuwafanyia wanyama majaribio ya kisayansi. Nilifikiri itakuwa ni njia salama kufanya kitu kizuri Lakini nina bahati mbaya hasa tulikamatwa wote. Polisi wakanipiga picha hii isiyoonekana vizuri Nikiwa nimeshika vipeperushi kama ushahidi.
My charges were dismissed, but a few weeks later, two FBI agents knocked on my door, and they told me that unless I helped them by spying on protest groups, they would put me on a domestic terrorist list. I'd love to tell you that I didn't flinch, but I was terrified, and when my fear subsided, I became obsessed with finding out how this happened, how animal rights and environmental activists who have never injured anyone could become the FBI's number one domestic terrorism threat.
Mashtaka kinyume nami yalifutwa, lakini wiki chache baadae, wanausalama wawili kutoka FBI wakaja nyumbani, wakaniambia kama sitawasaidia kwa kufanya upelelezi katika makundi ya waandamanaji Wataniweka katika orodha ya magaidi wa nyumbani Napenda nikwambie kuwa sikuogopa, lakini nilishtuka, Mshtuko wangu ulipoisha, Nilipata hamu ya kutaka kujua ,hali hii imefikaje hapa Jinsi wanaharakati wa haki za jamii na mazingira ambao hawajawahi kumjeruhi mtu yeyote wanaweza kuwa watu wa kwanza kwa shirika la FBI kuwafanya kuwa ni tishio kubwa la kiadui la nyumbani
A few years later, I was invited to testify before Congress about my reporting, and I told lawmakers that, while everybody is talking about going green, some people are risking their lives to defend forests and to stop oil pipelines. They're physically putting their bodies on the line between the whalers' harpoons and the whales. These are everyday people, like these protesters in Italy who spontaneously climbed over barbed wire fences to rescue beagles from animal testing. And these movements have been incredibly effective and popular, so in 1985, their opponents made up a new word, eco-terrorist, to shift how we view them. They just made it up.
miaka michache baadae, niliitwa kutoa ushahidi mbele ya bunge kuhusu ripoti yangu, na nikawaambia wabunge , kuwa wakati kila mtu anaongelea mapinduzi ya kijani, watu wengine wanatoa maisha yao kuilinda misitu na kuzuia mabomba ya mafuta. Wanaweka miili yao kati ya mitego ya nyangumi na nyangumi. Hawa ni watu wa kawaida, Kama waandamanaji hawa wa Italia ambao walipanda uzio wa waya kuwaokoa wanyama wasitumika katika majaribio ya kisayansi. na wimbi hili limekuwa la mafanikio sana na maarufu, Kwa hiyo mwaka 1985, wapinzani wao wakatengeneza neno jipya Gaidi wa mazingira, Ili kubadilisha jinsi tunavyowaona. walitengeneza tuu.
Now these companies have backed new laws like the Animal Enterprise Terrorism Act, which turns activism into terrorism if it causes a loss of profits. Now most people never even heard about this law, including members of Congress. Less than one percent were in the room when it passed the House. The rest were outside at a new memorial. They were praising Dr. King as his style of activism was branded as terrorism if done in the name of animals or the environment.
sasa kampuni hizi zimesaidia sheria mpya Kama Animal Enterprise Terrorism Act, ambayo inabadilisha uanaharakati kuwa ugaidi Kama itasababisha ukosefu wa faida. watu wengi hawajawahi hata kuisikia sheria hii, wakiwemo wabunge, Chini ya asilimia moja walikuwa bungeni ilipopitishwa Wengine walikuwa katika kumbukumbu wakimsifu Dr . King ambaye aina yake ya uanaharakati ingeitwa ugaidi kama ingefanywa kwa wanyama au mazingira.
Supporters say laws like this are needed for the extremists: the vandals, the arsonists, the radicals. But right now, companies like TransCanada are briefing police in presentations like this one about how to prosecute nonviolent protesters as terrorists. The FBI's training documents on eco-terrorism are not about violence, they're about public relations. Today, in multiple countries, corporations are pushing new laws that make it illegal to photograph animal cruelty on their farms. The latest was in Idaho just two weeks ago, and today we released a lawsuit challenging it as unconstitutional as a threat to journalism.
Waungaji mkono wanasema sheria hizi zinahitajika Kwa ajili ya wale wenye msimamo mkali wahuni na wanaoharibu mali. Lakini kwa sasa, kampuni kama TransCanada wanawaelekeza polisi jinsi ya kuwashtaki waandamanaji wa amani kama magaidi. Mafunzo ya FBI kuhusu ugaidi wa mazingira sio kwa ajili ya kuzuia vurugu ni kwa ajili ya mahusiano ya umma leo, katika nchi nyingi , mashirika makubwa yanalazimisha sheria mpya ambazo zinafanya kuwa kinyume na sheria upigaji picha wa ukatili wa wanyama katika mashamba yao. Habari ya karibuni kabisa ni huko idaho ,wiki mbili zilizopita, na leo tumefungua kesi tukisema ni kinyume na katiba na pia kama kitisho kwa uandishi wa habari
The first of these ag-gag prosecutions, as they're called, was a young woman named Amy Meyer, and Amy saw a sick cow being moved by a bulldozer outside of a slaughterhouse as she was on the public street. And Amy did what any of us would: She filmed it. When I found out about her story, I wrote about it, and within 24 hours, it created such an uproar that the prosecutors just dropped all the charges.
Mwanzo wa sheria hizi kufanya kazi ilikuwa ni pale binti aitwaye Amy Meyer, alipoona ng'ombe mgonjwa akiwa anahamishwa na tingatinga nje ya nyumba ya kuchinjia alipokuwa mtaani amy alifanya kile ambacho wengi wetu wangefanya: alipiga video. Nilipogundua habari,niliiandika Ndani ya masaa 24, ikaleta rabsha iliyosababisha mashtaka yote kufutwa.
But apparently, even exposing stuff like that is a threat. Through the Freedom of Information Act, I learned that the counter-terrorism unit has been monitoring my articles and speeches like this one. They even included this nice little write-up of my book. They described it as "compelling and well-written." (Applause) Blurb on the next book, right?
Lakini, hata kufichua mambo kama hayo ni tishio. Kupitia sheria ya uhuru wa mawasiliano Niligundua kuwa kitengo cha kudhibiti ugaidi kimekuwa kikifuatilia makala zangu Na hotuba kama hii. Hata wametoa maelezo haya kuhusu kitabu changu Wanaeleza kuwa "inavutia na imeandikwa vizuri" (Makofi) Muhtsari kuhusu kitabu kifuatacho, si ndio?
The point of all of this is to make us afraid, but as a journalist, I have an unwavering faith in the power of education. Our best weapon is sunlight.
Haya yote ni kutufanya tuogope, Lakini kama mwandishi wa habari,nina imani thabiti kuhusu nguvu ya elimu. Silaha yetu nzuri ni mwanga wa jua
Dostoevsky wrote that the whole work of man is to prove he's a man and not a piano key. Over and over throughout history, people in power have used fear to silence the truth and to silence dissent. It's time we strike a new note.
Dostoevsky aliandika kuwa kazi yote ya mtu ni kuthibitisha kuwa ni mtu na sio sehemu ya kinanda Mara nyingi katika historia Watawala wametumia uoga Kunyamazisha ukweli na upinzani Ni wakati wa kuanzisha kitu kipya
Thank you.
Asante Sana
(Applause)
(Makofi)