I would like to share with you a new model of higher education, a model that, once expanded, can enhance the collective intelligence of millions of creative and motivated individuals that otherwise would be left behind. Look at the world. Pick a place and focus on it. You will find humans chasing higher education. Let's meet some of them.
Ningependa kuwashirikisha muundo mpya wa helimu ya juu muundo ambao ukipanuliwa unaweza ukaongeza akili ya pamoja ya mamilioni ya watu binafsi walio na motisha na ubunifu ambao vinginevyo wange achwa nyuma. tazama ulimwengu chagua mahali na upaangazie utapata wanadamu wakikimbizana na elimu ebu tukutane na wengine wao
Patrick. Patrick was born in Liberia to a family of 20 children. During the civil war, he and his family were forced to flee to Nigeria. There, in spite of his situation, he graduated high school with nearly perfect grades. He wanted to continue to higher education, but due to his family living on the poverty line, he was soon sent to South Africa to work and send back money to feed his family. Patrick never gave up his dream of higher education. Late at night, after work, he surfed the net, looking for ways to study.
Patrick Patrick alizaliwa Liberia kwa familia ya watoto ishirini Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe, yeye na familia yake walilazimika kukimbilia Nigeria. huko licha ya hali yake, alihitimu sekondari kwa karibu alama kamili. Alitaka kuendelea na elimu ya juu lakini kutokana na familia yake kuishi katika mstari wa umaskini haikuchukua mda, akatumwa Afrika Kusini kufanya kazi na kutuma fedha nyumbani kulisha familia yake. Patrick hakuiacha ndoto ya elimu ya juu. usiku wa manane, baada ya kazi alipekua mtandao akitafuta njia za kusoma.
Meet Debbie. Debbie is from Florida. Her parents didn't go to college, and neither did any of her siblings. Debbie has worked all her life, pays taxes, supports herself month to month, proud of the American dream, a dream that just won't be complete without higher education. But Debbie doesn't have the savings for higher education. She can't pay the tuition. Neither could she leave work.
Kutana na Debbie. Debbie anatoka Florida. Wazazi wake hawakuenda chuo, wala yeyote wa ndugu zake. Debbie amefanya kazi maisha yake yote, hulipa kodi, na kujimudu mwezi kwa mwezi, akijivunia ndoto ya Marekani, ndoto ambayo haiwezi ikawa kamili bila elimu ya juu. Lakini Debbie hajaweka akiba ya elimu ya juu. hawezi kulipia masomo, wala kuweza kuacha kazi.
Meet Wael. Wael is from Syria. He's experiencing firsthand the misery, fear and failure imposed on his country. He's a big believer in education. He knew that if he could find an opportunity for higher education, an opportunity to get ahead of the rest, he has a better chance to survive in a world turned upside down.
Kutana na Wael. Wael ni mkaaji wa Syria. anapitia ana kwa ana taabu, hofu na kushindwa zilizowekewa nchi yake. Anaamini sana kwa elimu. Alijua kwamba akipata fursa ya elimu ya juu, fursa ya kutangulia wengine, ana nafasi nzuri ya kuishi
The higher education system
katika dunia iliogeuka kichwa chini.
failed Patrick, Debbie and Wael, exactly as it is failing millions of potential students -- millions that graduate high school, millions that are qualified for higher education, millions that want to study yet cannot access it for various reasons. First: financial. Universities are expensive; we all know it. In large parts of the world, higher education is unattainable for an average citizen. This is probably the biggest problem facing our society. Higher education stopped being a right for all and became a privilege for the few.
Mfumo wa elimu ya juu ulifeli Patrick, Debbie na Wael, jinsi tu inavyofeli mamilioni ya wanafunzi mamilioni waliohitimu shule za sekondari mamilioni ambao wamefuzu elimu ya juu mamilioni wanaotaka kusoma bali hawawezi wakapata kwa sababu tofauti. Kwanza, za fedha. Vyuo vikuu ni ghali. sote twajua Maeneo kubwa ulimwenguni elimu ya juu haiwezekani kwa raia wa kawaida. Hii ndio pengine shida kubwa inayokumba jamii yetu elimu ya juu ilikoma kuwa haki kwa wote
Second: cultural. Students who are qualified for higher education can afford -- want to study -- cannot, because it is not decent, it is not a place for a woman. This is the story of countless women in Africa, for example, prevented from higher education because of cultural barriers. And here comes the third reason: UNESCO stated that in 2025, 100 million students will be deprived of higher education, simply because there will not be enough seats to accommodate them, to meet the demand. They will take a placement test, they will pass it, but they still won't have access, because there are no places available.
ikawa teule kwa wachache. Pili, tamaduni. wanafunzi waliohitimu elimu ya juu, wanaojimudu, wanataka masomo, hawawezi Kwa sababu haiheshimiki, si mahali pa mwanamke. Hii ndio taswira ya mamia ya wanawake Afrika, Kwa mfano, Waliozuiliwa kwa elimu ya juu kwa sababu ya kinga za tamaduni. Na hapa ni sababu ya tatu: UNESCO ilisema kuwa mwakani 2025, wanafunzi milioni mia moja watanyimwa elimu ya juu kwa sababu tu, ya kutokua na viti tosha kuwapa malazi, kukidhi mahitaji. Watafanya mtihani wa usajili, wataupita, lakini bado hawatapata kuingia
These are the reasons I founded University of the People,
kwa sababu hakuna nafasi zilizoko
a nonprofit, tuition-free, degree-granting university to give an alternative, to create an alternative, to those who have no other; an alternative that will be affordable and scalable, an alternative that will disrupt the current education system, and open the gates to higher education for every qualified student regardless of what they earn, where they live, or what society says about them. Patrick, Debbie and Wael are only three examples out of the 1,700 accepted students from 143 countries.
Hizi ndizo sababu Nilianzisha Chuo kikuu cha watu, si cha faida, na bila malezi, Chuo kinachopeana shahada ya digrii kupeana mbadala, kujenga mbadala kwa wasio na mwingine mbadala ulio nafuu na wenye kipimo mbadala utakao koroga mfumo wa elimu wa sasa ufungue milango ya elimu ya juu kwa mwanafunzi yeyote aliyehitimu bila kujali pato lao, wala wanakoishi, ama jamii inavyonena kuwahusu. Patrick, Debbie na Wael ni mifano tatu tu kati ya wanafunzi 1,700 waliokubaliwa kutoka nchi 143.
(Applause) Thank you.
Sisi - (Makofi) - Asanteni.
(Applause)
We didn't need to reinvent the wheel. We just looked at what wasn't working and used the amazing power of the Internet to get around it. We set out to build a model that will cut down almost entirely the cost of higher education. And that's how we did it. First, bricks and mortar cost money. Universities have expenses that virtual universities don't. We don't need to pass these expenses on to our students. They don't exist. We also don't need to worry about capacity. There are no limits of seats in virtual university. Actually, nobody needs to stand at the back of the lecture hall. Textbooks are also something our students don't need to buy. By using open educational resources and the generosity of professors who are putting their material up free and accessible, we don't need to send our students to buy textbooks. All of our materials come free.
Hatukuitaji kuibuka na gurudumu jipya. Tuliangalia tu ni kipi kilikuwa hakifaulu na kutumia nguvu ya ajabu ya intaneti kukizingira. Tuliamua kujenga muundo utakao punguza kwa kiwango kikubwa gharama ya elimu ya juu na hivyo ndivyo tulifanya. Kwanza, matofali na chokaa ni gharama. Vyuo vikuu vina matumizi ambayo vyuo vikuu vya mtandao havina. Hatuitaji kupasha gharama hizi kwa wanafunzi wetu. Hazipo. Pia hatufai kubabaishwa na uwezo. hakuna mipaka ya viti kwa vyuo vikuu vya mtandao. Hakika, hakuna anayeitaji kusimama nyuma ya ukumbi. Vitabu vya kiada pia ni kitu wanafunzi wetu hawaitaji kununua. Kwa kutumia raisilimali za elimu ya wazi na ukarimu wa maprofesa wanaoweka nyenzo zao bure na zinapatikana, Hatuitaji kutuma wanafunzi wetu kununua vitabu vya kiada, nyenzo zetu zote zinakuja bure
Even professors, the most expensive line in any university balance sheet, come free to our students. Over 3,000 of them, including presidents, vice chancellors, professors and academic advisers from top universities such as NYU, Yale, Berkeley and Oxford, came on board to help our students.
hata maprofesa, Ule mustari ghali kabisa kwa mizania ya chuo kikuu chochote, huja bure kwa wanafunzi wetu, zaidi ya 3,000 yao wakiwemo Marais, makamu wa machancellor, maprofesa na washauri wa kitaaluma kutoka vyuo vikuu kama vile NYU, Yale, Berkely, na Oxford, wakajiunga nasi kuwasaidia wanafunzi wetu.
Finally, is our belief in peer-to-peer learning. We use this sound pedagogical model to encourage our students from all over the world to interact and study together, and also to reduce the time our professors need to labor over class assignments.
Hatimaye, ni imani yetu kwa masomo ya rika kwa rika. Tunatumia huu muundo wa ufundishaji imara kuwapa moyo wanafunzi kutoka kote duniani kuingiliana na kujifunza pamoja na pia kupunguza mda Maprofesa wetu wanaohitaji kujizatiti kwa kazi ya mazoezi darasani.
If the Internet has made us a global village, this model can develop its future leadership. Look how we do it. We only offer two programs: business administration and computer science, the two programs most in demand worldwide, the two programs that are likeliest to help our students find a job. When our students are accepted, they are placed in a small classroom of 20 to 30 students, to ensure that those who need personalized attention get it. Moreover, for every nine-week course, they meet a new peer, a whole new set of students from all over the world. Every week, when they go into the classroom, they find the lecture notes of the week, the reading assignment, the homework assignment, and the discussion question, which is the core of our studies. Every week, every student must contribute to the class discussion, and also must comment on the contribution of others. This way, we open our students' minds, we develop a positive shift in attitude toward different cultures. By the end of each week, the students take a quiz, hand in their homework, which are assessed by their peers under the supervision of the instructors, get a grade, move to the next week. By the end of the course, they take the final exam, get a grade, and follow to the next course.
Kama intaneti imetufanya kijiji cha kimataifa, muundo huu unaweza kuuendeleza uongozi wake wa usoni. Angalia vile tunavyoifanya. Tunatoa mipango miwili tu: utawala kibiashara na sayansi ya kompyuta, hiyo mipango miwili ndio inayosakwa sana duniani kote, hiyo mipango miwili ndio yenye uwezo mkubwa kuwasaidia wanafunzi wetu kupata ajira. Wanafunzi wetu wanapokubalika, huwekwa kwa darasa dogo la wanafunzi 20 kwenda 30 kuhakikisha wanaohitaji usaidizi binafsi wanapata. Zaidi ya hayo, kwa kila kozi ya wiki tisa, hukutana na rika mpya, kundi nzima la wanafunzi wapya kutoka kote ulimwenguni. Kila wiki, wanapoingia darasani, wanapata maelezo ya hotuba ya wiki, zoezi la kusoma, zoezi la ziada, na swali la majadiliano, ambayo ni msingi wa masomo yetu, Kila wiki, kila mwanafunzi lazima achangie kwa mjadala darasani na pia lazima atoe maoni kwa michango ya wengine. Kwa njia hii, tunafungua akili za wanafunzi wetu, tunakuza mwelekeo chanya kuelekea tamaduni tofauti. Mwisho wa kila wiki, wanafunzi hufanya jaribio, wanawasilisha kazi za ziada, ambazo hukaguliwa na wenzao kwa usimamizi wa waalimu, pata alama, enda kwa wiki nyingine. Mwisho wa kozi, hufanya mtihani wa mwisho, pata alama, na kuenda kwa kozi nyingine.
We open the gates for higher education for every qualified student. Every student with a high school diploma, sufficient English and Internet connection can study with us. We don't use audio, we don't use video. Broadband is not necessary. Any student from any part of the world with any Internet connection can study with us. We are tuition free. All we ask our students to cover is the cost of their exams, 100 dollars per exam. A full-time bachelor's degree student taking 40 courses will pay 1,000 dollars a year, 4,000 dollars for the entire degree. And for those who cannot afford even this, we offer them a variety of scholarships. It is our mission that nobody will be left behind for financial reasons. With 5,000 students in 2016, this model is financially sustainable.
Tulifungua milango ya elimu ya juu kwa mwanafunzi yeyote aliyehitimu. Mwanafunzi yeyote aliyehitimu sekondari, kingereza tosha na muunganisho wa intaneti anaweza kusoma na sisi. Hatutumii redio. Hatutumii video. upana wa bendi si hoja. Mwanafunzi yeyote kutoka kokote duniani aliye na mwuunganisho wowote wa intaneti anaweza kusoma nasi. tuko malezi-huru. tuulizacho tu wanafunzi wetu kukidhi ni gharama ya mitihani yao, Dola 100 kwa kila mtihani. Mwanafunzi wa muda kamili wa digrii ya hahada ya kwanza anayechukua kozi 40, atalipa dola 1,000 kwa mwaka, Dola 4,000 kukamilisha digrii, na kwa wale hawawezi kumudu hata hii, tunawapa udhamini aina mbali mbali. Ni dhamira yetu kuwa hakuna atakayeachwa nyuma kwa sababu za kifedha. Kwa wanafunzi 5,000 mwaka wa 2016, muundo huu ni endelevu kifedha.
Five years ago, it was a vision. Today, it is a reality. Last month, we got the ultimate academic endorsement to our model. University of the People is now fully accredited.
Miaka mitano iliyopita, yalikuwa maono. Leo, ni halisi. Mwezi jana, hatimaye tulipata muhuri wa kitaaluma kwa muundo wetu. Chuo kikuu cha watu sasa kina kibali rasmi
(Applause)
(Makofi)
Thank you.
Asanteni.
(Applause)
With this accreditation, it's our time now to scale up. We have demonstrated that our model works. I invite universities and, even more important, developing countries' governments, to replicate this model to ensure that the gates of higher education will open widely. A new era is coming -- an era that will witness the disruption of the higher education model as we know it today, from being a privilege for the few to becoming a basic right, affordable and accessible for all.
Kwa kibali hichi, ni wakati wetu sasa kupaa Tumeonyesha kwamba muundo wetu unafanya kazi. nakaribisha vyuo vikuu, na maana zaidi, serikali za nchi zinazokua, kuiga muundo huu kuhakikisha milango ya elimu ya juu itapanuka zaidi. Enzi mpya inakuja enzi itakayo shuhudia kuvurugika kwa elimu ya juu kama tunvyoijua leo, kutoka kuwa teule kwa wachache kuenda kuwa haki ya kimsingi, nafuu na inayopatikana kwa wote,
Thank you.
Asanteni.
(Applause)
(Makofi)