I thought I'd tell you a little about what I like to write. And I like to immerse myself in my topics. I just like to dive right in and become sort of a human guinea pig. And I see my life as a series of experiments.
Nimeona niwaeleze kidogo kuhusu kile ninachopenda kuandika Napenda kujikita hasa katika mada zangu. Napenda kuzamia humo na kuwa kama nguruwe. ninaona maisha yangu kama mkusanyiko wa majaribio
So, I work for Esquire magazine, and a couple of years ago, I wrote an article called "My Outsourced Life," where I hired a team of people in Bangalore, India, to live my life for me. So, they answered my emails. They answered my phone. They argued with my wife for me, and they read my son bedtime stories. It was the best month of my life, because I just sat back and I read books and watched movies. It was a wonderful experience.
Nafanya kazi na Jarida la Esquire, na miaka michache iliyopita Niliandika makala iliyoitwa "Maisha yangu kwenda kwa wengine" ambapo niliajiri watu katika mji wa Bangalore, India Kuyaishi kwa niaba yangu Kwa hiyo walikuwa wanajibu barua pepe zangu walijibu simu zangu Waligombana na mke wangu kwa niaba yangu,na kumsomea hadithi mtoto wangu wa kiume ulikuwa ni mwezi mzuri sana wa maisha yangu Kwa sababu nilikaa tu nikisoma vitabu na kuangalia filamu Hii ilikuwa hali nzuri sana
More recently, I wrote an article for Esquire called -- about radical honesty. And this is a movement where -- this is started by a psychologist in Virginia, who says that you should never, ever lie, except maybe during poker and golf, his only exceptions. And, more than that, whatever is on your brain should come out of your mouth. So, I decided I would try this for a month. This was the worst month of my life. (Laughter) I do not recommend this at all. To give you a sense of the experience, the article was called, "I Think You're Fat." (Laughter) So, that was hard.
Hivi karibuni, nimeandika makala kwa ajili ya jarida la Esquire Kuhusu kuwa mwaminifu hasa Na huu ni muunganiko wa watu ulioanzishwa na mwanasaikolojia katika mji wa Virginia Ambaye anasema usiseme uongo kabisa. labda tu wakati unacheza kamari au mchezo wa golf. Na zaidi ya hapo, chochote kilicho katika ubongo wako kinatakiwa kitoke katika mdomo wako Niliamua kuwa nitajaribu kwa mwezi mmoja. Huu ulikuwa ni mwezi mbaya sana wa maisha yangu (Vicheko) Sipendekezi hatua hii kwa mtu yeyote Kukujulisha jinsi hali inavyokuwa, Makala iliitwa "Nafikiri wewe ni mnene" (Vicheko) Kwa hiyo,ilikuwa ngumu
My most recent book -- my previous book was called "The Know-It-All," and it was about the year I spent reading the Encyclopedia Britannica from A to Z in my quest to learn everything in the world, or more precisely from Aak, which is a type of East Asian music, all the way to Zwyiec, which is -- well, I don't want to ruin the ending. (Laughter) It's a very exciting twist ending, like an O. Henry novel, so I won't ruin it. But I love that one, because that was an experiment about how much information one human brain could absorb. Although, listening to Kevin Kelly, you don't have to remember anything. You can just Google it. So, I wasted some time there.
Kitabu cha karibuni, kitabu cha zamani kinaitwa "kujua yote" Ulikuwa ni mwaka niliosoma kitabu cha Encyclopedia Britannica. Kutokea mwanzo mpaka mwisho, katika nia yangu ya kujifunza kila kitu katika Dunia au pia kutoka A-ak ambao ni aina ya muziki kutoka Mashariki ya Asia. Mpaka Zwyiec,ambayo ni -- sitaki kuharibu mwisho wake. (Vicheko) Ina mabadiliko ya ajabu mwishoni kama kitabu cha hadithi cha Henry, kwa hiyo sitaki kuharibu. lakini naipenda hiyo Kwa sababu hili lilikuwa ni zoezi kuhusu taarifa kiasi gani. ubongo mmoja unaweza kuchukua, ingawa ukimsikiliza Kevin Kelly, hauhitaji kukumbuka chochote. unaweza ukaitafuta katika mtandao wa Google kwa hiyo nilipoteza muda kidogo hapo
I love those experiments, but I think that the most profound and life-changing experiment that I've done is my most recent experiment, where I spent a year trying to follow all of the rules of the Bible, "The Year of Living Biblically." And I undertook this for two reasons. The first was that I grew up with no religion at all. As I say in my book, I'm Jewish in the same way the Olive Garden is Italian. (Laughter) So, not very. But I've become increasingly interested in religion. I do think it's the defining issue of our time, or one of the main ones. And I have a son. I want to know what to teach him. So, I decided to dive in head first, and try to live the Bible.
nayapenda majaribio kama hayo lakini nadhani jaribio muhimu zaidi na lililobadilisha maisha yangu ni hili la karibuni, ambapo nilikaa mwaka moja nikijitahidi kufuata maelekezo ya Biblia "Mwaka wa kuishi Kibiblia" na nilifanya hivi kwa sababu mbili Kwanza, ni kwa sababu nilikua bila dini kabisa Kama navyosema katika kitabu changu, ni Myahudi kama vile Kama vile bustani ya mizeituni ilivyo ya kiitaliano (vicheko) Kwa hiyo sio sana Lakini nimevutiwa sana na dini Na amini ni jambo muhimu sana kwa kipindi hiki moja muhimu kati ya mengi Na nina mtoto wa kiume na nataka nijue jinsi ya kumfundisha. kwa hiyo nikaamua kuishi kwa kufuata Biblia
The second reason I undertook this is because I'm concerned about the rise of fundamentalism, religious fundamentalism, and people who say they take the Bible literally, which is, according to some polls, as high as 45 or 50 percent of America. So I decided, what if you really did take the Bible literally? I decided to take it to its logical conclusion and take everything in the Bible literally, without picking and choosing.
Sababu ya pili ni kuwa ninaguswa na mwongezeko wa uhafidhina uhafidhina wa kidini, na watu wanaosema Wanaifuata Biblia kama ilivyo, na kwa mujibu wa tafiti mbalimbali Asilimia karibu 45 au 50 ya wamarekani Kwa hiyo nikaamua, itakuwaje kama utaifuata Biblia kama ilivyo? nikaamua kuifuata kufuata kila kama kilivyo bila kuchuja wala kubagua
The first thing I did was I got a stack of bibles. I had Christian bibles. I had Jewish bibles. A friend of mine sent me something called a hip-hop bible, where the twenty-third Psalm is rendered as, "The Lord is all that," as opposed to what I knew it as, "The Lord is my shepherd."
Kitu cha kwanza nilichofanya ilikuwa ni kutafuta Biblia nyingi Nilikuwa na Biblia ya Kikristo Nilikuwa na Biblia ya Kiyahudi Rafiki yangu alinitumia Biblia ya kufoka foka, Ambayo Zaburi ya 23, inasema "Bwana ndiye kila kitu", Badala ya "Bwana ndiye mchungaji wangu" kama ninavyojua
Then I went down and I read several versions, and I wrote down every single law that I could find. And this was a very long list -- over 700 rules. And they range from the famous ones that I had heard of -- The Ten Commandments, love your neighbor, be fruitful and multiply. So I wanted to follow those. And actually, I take my projects very seriously, because I had twins during my year, so I definitely take my projects seriously.
Na nikaendelea na kusoma tafsiri mbalimbali Na nikaandika kila agizo ambalo niliweza kuliona hii ilikuwa orodha ndefu -- zaidi ya maagizo 700 Kuanzia yale maarufu ambayo niliwahi kuyasikia Amri kumi, mpende jirani yako,enendeni mkaijaze nchi. Kwa hiyo nikataka kuzifuata Na kwa kweli nilichukulia jambo kwa uzito sana Kwa sababu nilipata watoto mapacha katika mwaka huo kwa hiyo nilichukulia jambo hili kwa uzito unaostahili
But I also wanted to follow the hundreds of arcane and obscure laws that are in the Bible. There is the law in Leviticus, "You cannot shave the corners of your beard." I didn't know where my corners were, so I decided to let the whole thing grow, and this is what I looked like by the end. As you can imagine, I spent a lot of time at airport security. (Laughter) My wife wouldn't kiss me for the last two months. So, certainly the challenge was there.
lakini pia nilitaka kufuata mamia ya maagizo ambayo hayajulikani na wengi ndani ya Biblia Kuna agizo katika Walawi Linalosema hauwezi kunyoa kona ya masharubu yako sikujua kona yangu itakuwa wapi, kwa hiyo nikaacha ziendelee kukua na hivi ndivyo nilivyokuwa mwishowe Na kama unavyoweza kufikiri, nilikuwa nasimamishwa sana na watu wa usalama katika viwanja vya ndege (Vicheko) Mke wangu hakutaka kunibusu katika miezi miwili ya mwisho Kwa kweli,ilikuwa ni changamoto
The Bible says you cannot wear clothes made of mixed fibers, so I thought, "Sounds strange, but I'll try it." You only know if you try it. I got rid of all my poly-cotton T-shirts. The Bible says that if two men are in a fight, and the wife of one of those men grabs the testicles of the other man, then her hand shall be cut off. So, I wanted to follow that rule. (Laughter) That one I followed by default, by not getting in a fight with a man whose wife was standing nearby, looking like she had a strong grip. (Laughter) So -- oh, there's another shot of my beard.
Biblia inasema hauwezi kuvaa nguo zinazotokana na mchanganyiko wa nyuzi kwa hiyo nikaona kuwa ni kitu kigeni lakini nikasema nitajaribu hauwezi kujua bila kujaribu nikaachana na fulana zangu za mchanganyiko mbalimbali Biblia inasema kama wanaume wawili wanapigana na mke wa mmoja wao akashika sehemu za siri za mwingine mkono wake unatakiwa ukatwe kwa hiyo nikataka nifuate agizo hilo (Vicheko) kwa hiyo nikalifuata bila kutaka kwa kutopigana na mwanaume ambaye mke wake alikuwa anasimama karibu, ambaye alionekana kama anaweza akanishika vizuri (Vicheko) na hii pia ni picha yangu nyingine ya sharubu zangu
I will say it was an amazing year because it really was life changing, and incredibly challenging. And there were two types of laws that were particularly challenging. The first was avoiding the little sins that we all commit every day. You know, I could spend a year not killing, but spending a year not gossiping, not coveting, not lying -- you know, I live in New York, and I work as a journalist, so this was 75, 80 percent of my day I had to do it.
ulikuwa ni mwaka wa ajabu kwa kuwa nilibadilishwa na pia ilikuwa ni changamoto ya ajabu kulikuwa na maagizo mawili ambayo yalinipa changamoto za kipekee Kwanza ilikuwa ni kujiepusha na dhambi ndogo tunazozifanya kila siku Ninaweza kukaa mwaka mzima bila kuua Lakini kukaa mwaka mzima bila kusengenya,bila kutamani,au kudanganya-- Ninaishi New York, na nafanya kazi kama mwandishi wa habari kwa hiyo asilimia 75, 80 ya siku ilibidi nifanye
But it was really interesting, because I was able to make some progress, because I couldn't believe how much my behavior changed my thoughts. This was one of the huge lessons of the year, is that I almost pretended to be a better person, and I became a little bit of a better person. So I had always thought, you know, "You change your mind, and you change your behavior," but it's often the other way around. You change your behavior, and you change your mind. So, you know, if you want to become more compassionate, you visit sick people in the hospital, and you will become more compassionate. You donate money to a cause, and you become emotionally involved in that cause. So, it really was cognitive psychology -- you know, cognitive dissonance -- that I was experiencing. The Bible actually talks about cognitive psychology, very primitive cognitive psychology. In the Proverbs, it says that if you smile, you will become happier, which, as we know, is actually true.
lakini ilikuwa ni ya kupendekeza, na nilifanikiwa kupiga hatua kwa kuwa sikuamini kwa kiasi gani matendo yangu yalibadilisha mawazo yangu ili lilikuwa ni somo kubwa sana kwa mwaka huo, ni kwamba nilijifanya kuwa mtu mzuri na nikafanikiwa kuwa mtu mzuri kidogo nimekuwa kila wakati nikifikiri, "Badilisha mawazo yako, na utabadilisha pia matendo yako, lakini mara nyingi inakuwa ni kinyume. Unabadilisha matendo yako, na pia unabadilisha mawazo yako. Kwa hiyo kama unataka kuwa mwema unatembelea wagonjwa hospitalini na utakuwa mwema unachangia pesa katika jambo fulani, na unajihusisha na jambo hilo kwa hiyo ilikuwa ni fikra za kisaikolojia unajua ilikuwa ni hali kutojisikia vizuri ambayo ilinikumba Biblia inaongelea kuhusu fikra za kisaikolojia fikra za kisaikolojia za kizamani sana Katika Mithali, inasema kama ukitabasamu,utakuwa na furaha. Ambavyo kama tunavyojua ni kweli
The second type of rule that was difficult to obey was the rules that will get you into a little trouble in twenty-first-century America. And perhaps the clearest example of this is stoning adulterers. (Laughter) But it's a big part of the Bible, so I figured I had to address it. So, I was able to stone one adulterer. It happened -- I was in the park, and I was dressed in my biblical clothing, so sandals and sort of a white robe, you know, because again, the outer affects the inner. I wanted to see how dressing biblically affected my mind. And this man came up to me and he said, "Why are you dressed like that?" And I explained my project, and he said, "Well, I am an adulterer, are you going to stone me?" And I said, "Well, that would be great!" (Laughter) And I actually took out a handful of stones from my pocket that I had been carrying around for weeks, hoping for just this interaction -- and, you know, they were pebbles -- but he grabbed them out of my hand. He was actually an elderly man, mid-70s, just so you know. But he's still an adulterer, and still quite angry. He grabbed them out of my hand and threw them at my face, and I felt that I could -- eye for an eye -- I could retaliate, and throw one back at him.
Aina ya pili ya agizo ambayo ilikuwa ngumu kufuata, Ilikuwa ni agizo ambalo litakuingiza katika matatizo kidogo Katika Marekani ya karne ya 21. Na mfano mzuri wa hii ni kuwapiga mawe wazinzi (Vicheko) Lakini ni sehemu kubwa ya Biblia Kwa hiyo nikaona ni vizuri niiongelee Kwa hiyo niliweza kumpiga mawe mzinzi mmoja ilitokea, nilikuwa katika bustani, na nilikuwa nimevaa mavazi yangu ya kibiblia sandoz na kanzu nyeupe kama unavyojua tena, nje kunaathiri ndani. Nilitaka kuona uvaaji wa kibiblia utaathiri vipi mawazo yangu na mtu mmoja akaja akaniambia Kwa nini umevaa hivyo? Nikamweleza kuhusu zoezi langu, Na akasema mimi ni mzinzi je utanipiga mawe? Nikasema, "nadhani hiyo itakuwa nzuri" (Vicheko) Nikachukua mawe kadhaa kutoka katika mfuko wangu ambayo nilikuwa nimeyabeba kwa wiki kadhaa nikitumaini kupata nafasi kama hii, na yalikuwa mawe madogo tu lakini aliyachukua kutoka katika mkono wangu alikuwa ni mtu mzima,katikati ya miaka sabini. lakini bado alikuwa ni mzinzi, na mwenye hasira aliyachukua kutoka mkononi mwangu akanirushia usoni, na nikahisi kuwa jicho kwa jicho, ningeweza kumrudishia, nikamrushia moja.
So that was my experience stoning, and it did allow me to talk about, in a more serious way, these big issues. How can the Bible be so barbaric in some places, and yet so incredibly wise in others? How should we view the Bible? Should we view it, you know, as original intent, like a sort of a Scalia version of the Bible? How was the Bible written? And actually, since this is a tech crowd, I talk in the book about how the Bible actually reminds me of the Wikipedia, because it has all of these authors and editors over hundreds of years. And it's sort of evolved. It's not a book that was written and came down from on high.
Kwa hiyo,huo ndio ulikuwa uzoefu wangu,kuhusu kupiga mawe,na uliniruhusu kuongelea kwa uzito zaidi mambo mazito haya Kwa nini Biblia ni ya kikatili katika sehemu nyingine, Na papo hapo imejaa hekima kupindukia katika maeneo mengine Tuiangalieje Biblia? Je tuiangalie katika dhumuni lake halisi Kama tafsiri ya Scalia ya Biblia? Je Biblia iliandikwaje? Na kwa kuwa hii ni hadhara ya watu wa teknolojia Ninaongelea katika kitabu jinsi Biblia ambavyo inanikumbusha, Kuhusu Wikipedia wa sababu ina waandishi na wahariri mbalimbali kwa zaidi ya mamia ya miaka Na imeendela kubadilika Sio kitabu kilichoandikwa na kushuka kutoka juu
So I thought I would end by telling you just a couple of the take-aways, the bigger lessons that I learned from my year. The first is, thou shalt not take the Bible literally. This became very, very clear, early on. Because if you do, then you end up acting like a crazy person, and stoning adulterers, or -- here's another example. Well, that's another. I did spend some time shepherding. (Laughter) It's a very relaxing vocation. I recommend it.
Nafikiri nimalizie kwa kuwaeleza kuhusu mambo makubwa niliyojifunza katika mwaka huu Cha kwanza, Usichukue neno katika Biblia bila kulielewa Hii ilikuwa dhahiri kwangu mwanzoni kabisa Kwa sababu kama ukifanya hivyo,utakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa kuwapiga mawe wazinzi au mfano mwingine nilikaa nikichunga kondoo (Vicheko) ni kazi nzuri, napendekeza kwa wengine
But this one is -- the Bible says that you cannot touch women during certain times of the month, and more than that, you cannot sit on a seat where a menstruating woman has sat. And my wife thought this was very offensive, so she sat in every seat in our apartment, and I had to spend much of the year standing until I bought my own seat and carried it around.
Lakini pia Biblia inasema hauwezi kumshika mwanamke akiwa katika siku zake za hedhi Hauruhusiwi kukaa katika kiti ambacho mwanamke aliye katika hedhi alikaa Mke wangu hakuipenda hii kwa hiyo akawa anakaa katika kila kiti katika nyumba yetu ilibidi niishi karibia mwaka wote nikiwa nasimama mpaka niliponunua kiti changu na kuwa nakibeba
So, you know, I met with creationists. I went to the creationists' museum. And these are the ultimate literalists. And it was fascinating, because they were not stupid people at all. I would wager that their IQ is exactly the same as the average evolutionist. It's just that their faith is so strong in this literal interpretation of the Bible that they distort all the data to fit their model. And they go through these amazing mental gymnastics to accomplish this.
nilikutana na watu wanaoamini kuhusu uumbaji nikaenda katika makumbusho ya watu hawa hawa ni wale wanaochukua maneno kama yalivyo ilipendeza sana, kwa kuwa hawakuwa wajinga kabisa. ufahamu wao ulikuwa ni sawa sawa na wale wasioamini juu ya uumbaji Tofauti ni kuwa imani ni kubwa sana Katika tafsiri hii ya Biblia ambayo imebadilishwa ili kwendana na mawazo yao Na wanabadilisha vitu ili kufanikisha hii.
And I will say, though, the museum is gorgeous. They really did a fantastic job. If you're ever in Kentucky, there's, you can see a movie of the flood, and they have sprinklers in the ceiling that will sprinkle on you during the flood scenes. So, whatever you think of creationism -- and I think it's crazy -- they did a great job. (Laughter)
Ingawa nitasema kuwa makumbusho ni nzuri sana. walifanya kazi nzuri sana kama itatokea kuwa Kentucky, Pale -- unaweza kuona filamu ya gharika, na wana vibomba vidogo vidogo katika dari ambavyo vitakumwagia maji katika sehemu ambayo filamu inaonyesha mafuriko Kwa hiyo vyovyote unavyofikiri kuhusu uumbaji walifanya kazi nzuri (Vicheko)
Another lesson is that thou shalt give thanks. And this one was a big lesson because I was praying, giving these prayers of thanksgiving, which was odd for an agnostic. But I was saying thanks all the time, every day, and I started to change my perspective. And I started to realize the hundreds of little things that go right every day, that I didn't even notice, that I took for granted, as opposed to focusing on the three or four that went wrong. So, this is actually a key to happiness for me, is to just remember when I came over here, the car didn't flip over, and I didn't trip coming up the stairs. It's a remarkable thing.
Somo jingine ni kuwa unatakiwa uwe ni mtu wa shukrani na hili lilikuwa ni somo kubwa kwa kuwa nilikuwa ninaomba nikitoa maombi ya shukrani, Nilikuwa nasema asante wakati wote, kila siku, nikaanza kubadilisha mtazamo wangu nikaanza kutambua vitu vidogo vidogo vingi ambavyo vinatokea kila siku, ambavyo sikuweza hata kuvijua ambavyo sikuvizingatia, toauti na kutiliaa maanani kati ya vitatu au vinne ambavyo havikwenda vizuri kwa huu ndiyo ufunguo wa furaha kwangu mimi ni kukumbuka kuwa nilipokuja hapa gari halikupinduka, na sikuteleza wakati napanda ngazi ni kitu cha ajabu sana
Third, that thou shall have reverence. This one was unexpected because I started the year as an agnostic, and by the end of the year, I became what a friend of mine calls a reverent agnostic, which I love. And I'm trying to start it as a movement. So, if anyone wants to join, the basic idea is, whether or not there is a God, there's something important and beautiful about the idea of sacredness, and that our rituals can be sacred. The Sabbath can be sacred. This was one of the great things about my year, doing the Sabbath, because I am a workaholic, so having this one day where you cannot work, it really, that changed my life. So, this idea of sacredness, whether or not there is a God.
Tatu,unatakiwa uwe na hofu ya Mungu Hii sikuitegemea, kwa sababu nilianza mwaka Kama mtu asiye na hakika na uwepo wa Mungu, lakini mwishoni mwa mwaka Nikawa kama rafiki yangu anavyopenda kusema,asiyeamini mwenye hofu ya Mungu,kitu ambacho nakipenda Na nataka nianzishe muungano wa watu wa namna hii kama mtu yoyote anataka kujiunga wazo kuu ni, kama Mungu yupo au la, Kuna kitu muhimu na kizuri kuhusu utakatifu na mambo yetu ya kila siku yanaweza yakawa matakatifu Sabato inaweza ikawa takatifu Hiki kile ni kitu kizuri sana katika mwaka huu kwa kuifuata Sabato Kwa sababu napenda sana kufanya kazi,kwa hiyo kupata hii siku moja ambayo haufanyi kazi ,ilibadilisha maisha yangu. Kwa hiyo wazo hili la utakatifu,bila kujali kama Mungu yupo au la,
Thou shall not stereotype. This one happened because I spent a lot of time with various religious communities throughout America because I wanted it to be more than about my journey. I wanted it to be about religion in America. So, I spent time with evangelical Christians, and Hasidic Jews, and the Amish. I'm very proud because I think I'm the only person in America to out Bible-talk a Jehovah's Witness. (Laughter) After three and a half hours, he looked at his watch, he's like, "I gotta go." (Laughter) Oh, thank you very much. Thank you. Bless you, bless you.
Usilidharau Hii imetokea kwa sababu kwa sababu natumia muda mwingi na jamii za dini mbalimbali katika maeneo mengi ya Marekani, na nilitaka pia iwe zaidi tu ya safari yangu Nilitaka iwe ni kuhusu dini nchini Marekani Kwa nakaa na wakristo waliookoka, na wayahudi. Ninajivunia kwa kuwa nadhani ni mtu pekee Marekani yote Kuongelea Biblia kumshinda Shahidi wa Yehova (Vicheko) Baada ya masaa matatu aliangalia saa yake, na akasema,"inabidi niondoke" (Vicheko) Asante sana Asante sana. mbarikiwe
But it was interesting because I had some very preconceived notions about, for instance, evangelical Christianity, and I found that it's such a wide and varied movement that it is difficult to make generalizations about it. There's a group I met with called the Red Letter Christians, and they focus on the red words in the Bible, which are the ones that Jesus spoke. That's how they printed them in the old Bibles. And their argument is that Jesus never talked about homosexuality. They have a pamphlet that says, "Here's what Jesus said about homosexuality," and you open it up, and there's nothing in it. So, they say Jesus did talk a lot about helping the outcasts, helping poor people. So, this was very inspiring to me. I recommend Jim Wallis and Tony Campolo. They're very inspiring leaders, even though I disagree with much of what they say.
lakini pia cha kuvutia ni kwa sababu nilikuwa na mawazo yangu mwenyewe kuhusu kwa mfano, Ukristo wa kuokoka, na nilikuja kujua Ni eneo pana na lenye tofauti mbalimbali Na hauwezi ukawa na maelezo ya jumla juu ya kundi hili Kuna nikundi nilikutana nacho kiitwacho Wakristo wa Barua nyekundu, Na wao wanaangalia maneno mekundu katika Biblia, Ambayo ndiyo yale yaliyotamkwa na Yesu ambayo ndivyo yalivyochapishwa katika Biblia za zamani. Na wao wanasema kuwa Yesu hakusema chochote kuhusu ushoga na usagaji. Wana kijarida ambacho kinasema, "hivi Ndivyo Yesu alivyosema kuhusu Usagaji na Ushoga" Na ukifungua,Hautakuta kitu chochote. Kwa hiyo wanasema Yesu aliongelea sana kuhusu kuwasaidia watu waliotengwa, Kuwasaidia maskini. Kwa hiyo ilikuwa changamoto kubwa kwangu. Ninawapendekeza kwenu Jim Wallace na Tony Campolo. Ni viongozi wanaotoa hamasa sana,ingawa sikubaliana, Na mengi wanayoyasema.
Also, thou shalt not disregard the irrational. This one was very unexpected because, you know, I grew up with the scientific worldview, and I was shocked learning how much of my life is governed by irrational forces. And the thing is, if they're not harmful, they're not to be completely dismissed. Because I learned that -- I was thinking, I was doing all these rituals, these biblical rituals, separating my wool and linen, and I would ask these religious people "Why would the Bible possibly tell us to do this? Why would God care?" And they said, "We don't know, but it's just rituals that give us meaning." And I would say, "But that's crazy." And they would say, "Well, what about you? You blow out candles on top of a birthday cake. If a guy from Mars came down and saw, here's one guy blowing out the fire on top of a cake versus another guy not wearing clothes of mixed fabrics, would the Martians say, 'Well, that guy, he makes sense, but that guy's crazy?'" So no, I think that rituals are, by nature, irrational. So the key is to choose the right rituals, the ones that are not harmful -- but rituals by themselves are not to be dismissed.
Pia hautakiwi kudharau kitu kisichoeleweka Hii sikuitegemea kwa kuwa Nimekulia katika ulimwengu wa sayansi, na nilishangaa kuona jinsi maisha yangu yanavyoongozwa na nguvu zisizoeleweka. Na kama kitu hakiumizi, si kitu cha kudharau moja kwa moja. Kwa sababu nimejifunza kuwa-- nilikuwa nafikiri kufanya mambo yote haya, ya Kibiblia, kutenganisha nguo zangu,na nilikuwa nikiwauliza watu wa dini, Kwa nini Biblia itueleze hivi?Kwa nini Mungu ajali? Na wakasema,"Hatujui, lakini ni mambo ambayo yanatupa sisi maana" Na nikawa nasema, "Lakini huu ni ujinga." na wao wakasema,"je vipi kuhusu wewe? unapuliza mishumaa iliyo juu ya keki ya siku ya kuzaliwa. Kama mtu kutoka sayari ya Mars akija na kuona mtu anapuliza moto juu ya keki na mtu mwingine ambaye havai mavazi ya vitambaa mchanganyiko Je watu hawa kutoka sayari ya Mars unafikiri watasema, "mtu huyu anafanya kitu cha kueleweka Lakini huyu anafanya ujinga?" Kwa hiyo nafikiri mapokeo mengi ni vitu visivyoeleweka. Kwa hiyo muhimu ni kuchagua mapokeo mazuri, yale ambayo hayakuumizi, lakini mapokeo yenyewe hayatakiwi kudharauliwa
And finally I learned that thou shall pick and choose. And this one I learned because I tried to follow everything in the Bible. And I failed miserably. Because you can't. You have to pick and choose. And anyone who follows the Bible is going to be picking and choosing. The key is to pick and choose the right parts. There's the phrase called cafeteria religion, and the fundamentalists will use it in a denigrating way, and they'll say, "Oh, it's just cafeteria religion. You're just picking and choosing." But my argument is, "What's wrong with cafeterias?" I've had some great meals at cafeterias. I've also had some meals that make me want to dry heave. So, it's about choosing the parts of the Bible about compassion, about tolerance, about loving your neighbor, as opposed to the parts about homosexuality is a sin, or intolerance, or violence, which are very much in the Bible as well. So if we are to find any meaning in this book, then we have to really engage it, and wrestle with it.
Na pia nilijifunza pia kuwa unatakiwa kuangalia vizuri na kuchagua. Na hii nilijifunza kwa sababu Nilijaribu kufuata kila kitu katika Biblia. Na nikashindwa vibaya sana Kwa kuwa haiwezekani. inabidi uchague, na yoyote anayeifuata Biblia atakuwa anachagua. Muhimu ni kuchagua sehemu muhimu. kuna msemo unaosema Dini ya mgahawa, watu wanaofuata sana dini wataisema katika hali ya kumshusha mtu, Kuwa ni " Dini ya mgahawa. Unachagua tu" lakini msimamo ni kuwa, " Kuna tatizo gani na migahawa?" Nimefanikiwa kula vyakula vizuri sana katika migahawa. lakini pia nimekula vyakula ambavyo vilinifanya nitake kutapika. Kwa hiyo, ni kuchagua sehemu za Biblia zinazohusu huruma, ma uvumilivu,kuhusu kuwapenda jirani zako, badala ya sehemu za ushoga na usagaji kuwa ni dhambi, au kukosa uvumilivu na machafuko. ambavyo vipo katika Biblia pia. Kama tunataka kupata maana katika kitabu hiki, tunahitaji kukitafakari hasa,
And I thought I'd end with just a couple more. There's me reading the Bible. That's how I hailed taxicabs. (Laughter) Seriously, and it worked. And yes, that was actually a rented sheep, so I had to return that in the morning, but it served well for a day. So, anyway, thank you so much for letting me speak.
Na nafikiri nimalizie na vitu vichache. hapa ni mimi nikisoma Biblia. Hivi ndivyo nilivyoziita teksi. (Vicheko) na ilifanya kazi huyo alikuwa ni kondoo wa kukodiwa, kwa hiyo ilibidi nimrudishe asubuhi, lakini ilinisaidia kwa siku moja, Kwa hiyo nashukuru sana kwa kuniruhusu kuongea nanyi.